NEW VIDEO (TANZANIA)- Linah athibitisha kuja na video mpya baada ya “No stress”

Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga ambaye anatamba na video yake ya No Stress, sasa anatarajia kuja na video ya single mpya iitwayo Happy Day inayoandaliwa na director wawili Hanscana na Khalfan. Kupitia tovuti ya Millard ayo  “ Nina ngoma yangu inaitwa HAPPY DAY, Soon itatoka. Video imefanywa na HANSCANA pamoja na KHALFAN” Linah.

Pia Linah aliongeza “Nimefanya na hawa madirector kwasababu naamini ni njia nzuri ya kuonekana kazi pia nje, hususani kwa sisi ambao tumepata nafasi za video zetu kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya nje”

“Kwenye hii ngoma nimefanya style flani kama ya kuchezeka, watu waendelee kusikiliza vitu vizuri Zaidi. Pia kuna kolabo moja nimefanya na msanii mkubwa AFRICA..!Watu wasubiri”. ;-Linah.

Leave your comment