EXCLUSIVE (TANZANIA) - Professor Jay ashinda kiti cha ubunge Mikumi
28 October 2015

Rapper wa muda mrefu na mkongwe, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amechaguliwa kuwa mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro.
Pr Jay ambaye alikuwa anawania ubunge kwa tiketi ya Chadema, ametangazwa rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo kwa kupata kura 32,259 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Jonas Nkya wa CCM aliyepata kura 30,425. Kwa mujibu wa ITV, msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mikumi amemtangaza rasmi Professor Jay kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.
Pia Professor Jay aliweka katika ukurasa wake wa Instagram habari hiyo njema kwa kuandika: Jimbo la Mikumi Joseph Haule (CHADEMA) kura 32,259, JONAS NKYA 30,425, Tumeshinda kwa tofauti ya kura 1834. Asante Mungu
Rapper huyo ambaye ni wa pili kuingia bungeni baada ya Joseph ‘sugu’ Mbilinyi aliyeshinda ubunge wa Mbeya mjini kwa mara ya pili.




Leave your comment