NEW RELEASE (TANZANIA)- Joh Makini, G-Nako, Nikki Wa Pili kuachia single 3 wiki ijayo.
23 October 2015

Wasanii kutoka kundi la weusi kuachia single 3 wiki ijayo baada ya uchaguzi, mbili kati ya hizo tayari zimefanyiwa video na Justine Campos.
Kwa muda wa miezi miwili iliyopita Joh Makini na G Nako walienda Afrika Kusini kushoot video mbili mpya, kati ya hizo moja ilikua kati ya Joh na rapper wa Afrika kusini AKA, “Don’t bother” na nyingine ni ya G Nako iitwayo “Original”
Nyimbo zote hizo mbili pamoja na ya Nikki wa Pili iitwayo “Baba Swalehe” zitatoka rasmi wiki ijayo japo hawajasema tarehe.
Kupitia istagram Joh Makini pia amepost,
“Baba swalehe @nikkwapili
Original@gnakowarawara
Don’t bother feat@akaworldwide
Produced by @nahreel #TheIndustry
Loading……”
Source:Bongo 5




Leave your comment