EXCLUSIVE (TANZANIA)- Wasanii tutumie umaarufu wetu vizuri –Jokate

Jokate Mwegelo ambaye ni mwanamitindo na muimbaji amewataka wasanii  kutumia umaarufu wao vizuri ili wapewe ushirikiano na kila mtu katika kazi zao. Ameyasema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa wasanii wengi wanavimba kichwa baada ya kupata umaarufu hali inayopelekea mwisho wao kuwa mbaya.

“Unajua ukiwa maarufu kila mtu akawa anaimba nyimbo yako, ni rahisi kuvimba kichwa ukajiona wewe ndio wewe, unasahau kabla ya wewe kulikuwa na watu ambao walihit vilevile. Hii ni cycle leo umehit wewe, kesho yule”.  Na kuongeza kuwa cha muhimu ni kufanya kazi kwa bidii na heshima.

Leave your comment