EXCLUSIVE (TANZANIA)- Kuwa na tuzo kunaongeza CV kwa msanii-Vanessa Mdee
21 October 2015

Mwanadada Vanessa ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya “Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki” AFRIMMA, amesema anaamini msanii anapopata tuzo nyingi haimaanishi ndiyo anafanya vizuri sana, na msanii kuwa na tuzo chache haimaanishi hafanyi vizuri.
“Msanii kuwa na Tuzo, kwa mfano tumuangalie Wizkid ana tuzo chache, lakini muziki wake unafanya vizuri dunia nzima, Drake anamtafuta, Swizbeat anamtafuta, Alicia Keys anamtafuta na ratiba yake ipo busy mwaka mzima, So haijalishi” alisema Vanessa.
Kuna sababu nyingi za msanii kutokukupata tuzo nyingi hata kama anapata nomination mara kwa mara kama Wizkid, ikiwa ni pamoja na kutojipigia kampeni ya kutosha kuweza kupata kura nyingi.
Source: Bongo5




Leave your comment