EXCLUSIVE (TANZANIA): Muziki wa Barakah Da’ Prince ulianzia hapa.. Diamond na post za Swizz Beatz !! Dully Sykes na Siasa..

Barakah Da’ Prince ni miongoni mwa wasanii waliopata changamoto kubwa wakati wakiingia kwenye sanaa muziki.. leo kafunguka kupitia 255 na kusema wakati anaanza sanaa hiyo alikua anaiba muda wake wa shule kwa kutoroka shule na kwenda studio akiwa pamoja na wenzake.. baba yake alikua akimfuatilia sana na kumpiga kutokana na kutohudhuria masomo, lakini kaka yake ndiye alikuwa mtu ambaye akimsaidia sana na kufanya baba yake amruhusu kufanya muziki.

NEW VIDEO (TANZANIA): Diamond And Vanessa Mdee Empower Women With The Remix To 'Strong Girl'


Mume wa Alicia Keys producer na rapper Swizz Beatz jana alipost video za mtoto wake akiwa anacheza wimbo wa ‘Nana‘ na ‘Nataka Kulewa‘ za Diamond Platnumz… 255 imempata Diamond leo, jamaa amesema alipata habari hiyo wakati akiwa studio.

EXCLUSIVE (TANZANIA): Swizz Beatz Jamming To Two Of Diamond Platnumz Singles!

Diamond anasema alijisikia vizuri sana na kuamua kumjibu kwa kumshukuru Swizz… Anasema hiyo kwake ni ishara kwamba muziki wa Tanzania una thamani na unatambulika Duniani.

 

 


Dully Sykes amefunguka kuhusu mwenendo wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu jinsi unavyokwenda na kusema yeye ni Mtanzania kama wengine na amepewa kipaji cha kuwa kioo cha jamii.. Dully amesema yeye hayupo chama chochote lakini kitendo cha wasanii kuwakebehi wanasiasa wakubwa sio vizuri kwa upande wake hajapenda na angependa kila mtu atambue kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi.

SOURCE: Millardayo.com

RELATED

 EXCLUSIVE (TANZANIA): Diamond Platnumz Spills About Zari To CNN!

Leave your comment