WANASOKA WA BRAZIL WALIOTUMIKIA JELA

WANASOKA WA BRAZIL WALIOTUMIKIA JELA

Taarifa mpya ya kusikitisha pale Brazil na Hispania kwa upande wa soka ni kifungo cha nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona, Dani Alves ambaye mwezi uliopita alihukumiwa kwenda jela miaka minne na nusu kwa kosa la ubakaji.

Leo mchezaji huyo aliyecheza soka kwa mafanikio makubwa, aliomba kuachiwa huru kwa muda huku akisubiri hatima ya rufaa yake aliyoiwasilisha, lakini ombi hilo limegonga mwamba huku mahakama ikiwa na hofu ya staa huyo mwenye miaka 40 kutoroka.

Achana na hukumu hiyo ya Alves, kutana na mastaa wengine wa nchini Brazil ambao walihukumiwa kwenda jela.

Ronaldinho Gaucho
Mchezaji pekee ambaye anatajwa kuwa aliupenda mpira na mpira ulimpenda zaidi na kumtii kila atakalo akiwa uwanjani. Alihukumiwa kwenda jela mwaka 2020 nchini Paraguay na kaka yake kwa kosa la utakatishaji wa fedha na kutumia ‘pasi feki’ ya kusafiria.

Hata hivyo mchezaji huyo ambaye aliwafanya mashabiki wengi wapende soka, alikaa jela kwa kipindi cha miezi mitano na kuachiwa huru.

Edson Cholbi
Huyu ni mtoto wa gwiji wa soka Brazil, Edson Pele, ambaye umaarufu wake ni kutokana na jina la baba yake, lakini alicheza soka katika klabu kadhaa bila mafanikio makubwa katika nafasi yake ya golikipa.

Naye alionja jota la jiwe mara kadhaa, ikiwa mwaka 2005 alikwenda jela kwa kosa la utapeli wa fedha na biashara za dawa za kulevya.

Breno Vinicius
Beki wa kati wa zamani wa Bayern Munich, yeye alitumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuchoma moto nyumba yake kwa kukusudia.

Robinho
Huyu naye anaweza kwenda kuitumikia jela miaka tisa kwa kosa kama lile la Alves, ubakaji. Huku ya mchezaji huyo itasikilizwa Jumatano wiki ijayo, ila yeye bado hajaonja kifungo kama wenzake.

Unadhani kwa nini mastaa wanafanya makosa kama haya bila kujali fedha walizonazo?

Leave your comment