Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii
6 June 2023
Picha Instagram
Imeandikwa na Charles Maganga
Kama unapenda ngoma mpya zenye mahadhi ya Bongo Fleva, Baibuda, Bongo Hip Hop au hata Swahili Amapiano basi makala hii ni kwa ajili yako kwani kupitia makala hii tunaenda kuzihesabu ngoma mpya kali kutoka Tanzania kwa wiki hii:
Kutoka kwa wasanii kama Nandy, Dayoo, Anjella na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma mpya Tanzania kwa wiki hii
Blessing - Anjella
Baada ya ukimya wa miezi kadhaa Anjella amerudi tena na “Blessing” ngoma kali ya Bongo Fleva ambapo ndani yake ametuhadithia kuhusu changamoto anazopitia kwa sasa bila kukata tamaa.
Raha - Nandy
“Raha” ni wimbo wa pili kutoka kwa Nandy kwa mwaka 2023 na bila shaka mashabiki wameupokea vizuri wimbo wenye mahadhi ya Bongo Fleva na ambao mashahiri yake yanahusu namna ambavyo Nandy anapata raha kwenye mapenzi
Manaake Nini - Freshboys
“Manaake Nini” ni ngoma ya kwanza kabisa kutoka kwa kundi hili la Hip Hop kutoka Bongo na bila shaka tangu ngoma hii iachiwe imepokelewa vyema sana na mashabiki pamoja na wadau tofauti tofauti wa muziki.
Unatosha - Dayoo
Kwenye mkwaju wake mpya Dayoo anamuhakikishia mpenzi wake kwamba ametosheka sana na kwamba hawezi kumuacha kamwe au kumuumiza hisia zake.
Rockabye Remix - Barnaba Ft Otile Brown
Barnaba na Otile wameamua kuunganisha nguvu ili kuileta kwa mashabiki “Rockabye Remix”. Kama unapenda melody kali pamoja na mashahiri mazuri ya Bongo Fleva basi Rockabye Remix ni kwa ajili yako.
Leave your comment