Zuchu Aungana Na Innos B Kwenye “Nani Remix”
2 June 2023
Picha: Instagram
Imeandikwa na Charles Maganga
Msanii nguli kutoka Tanzania, Zuchu kwa mara nyingine ameamua kukosha mashabiki zake baada ya kuachia remix ya wimbo wake wa “Nani” ambao amemshirikisha Innos B
Zuchu aliachia “Nani” takriban wiki 3 zilizopita kwa mapokezi makubwa ambapo mashabiki wengi wa muziki wameonekana kupenda ngoma hiyo ambayo imetayarishwa na producer S2kizzy
Kwenye “Nani Remix” Innos B ameongeza ladha ya kikongo kwenye mdundo huo ambapo pia amesikika akiimba kwa lugha ya Kikongo. Zuchu kwa upande wake, amekoleza “Nani Remix” na sauti yake mujarab pamoja na mashahiri mepesi yasiyochosha.
Hii si mara ya kwanza kwa Zuchu na Innos B kushirikiana kwenye ngoma ya pamoja. Miezi mitatu iliyopita wawili hao walikutana pamoja kwenye ngoma ya “Kiss” ya kwake Innos B.
Leave your comment