NYIMBO ZINAZOTAMBA TANZANIA WIKI HII

Picha Instagram
Imeandikwa na Charles Maganga

Kama ulikuwa unajiuliza ni ngoma gani ambazo zinafanya vizuri zaidi nchini Tanzania kwa wiki hii basi itoshe kusema kuwa makala hii ni kwa ajili yako.

Kutoka kwa wasanii ksma Mbosso, Nandy, Marioo na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma tano zinazofanya vizuri zaidi Tanzania kwa wiki hii:

Amepotea - Mbosso

Amepotea ya Mbosso imeonesha ni kwa namna gani, msanii huyo kutokea WCB ana kipaji cha uandishi na bila shaka mashabiki wameipokea kwa mikono miwili ngoma hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2.9 tangu kuachiwa kwakeTomorrow - Marioo

Linapokuja la Amapiano kwa lugha ya Kiswahili, fundi mara nyingi huwa ni mmoja tu, naye ni Marioo na kupitia mkwaju wake wa “Tomorrow” Marioo ameweza kuthibitisha hiloFalling - Nandy

Video ya “Falling” ya kwake Nandy inastahili tuzo kwa ubunifu mkubwa uliotumika ndani ya video hii ambayo kwa sasa imeteka hisia na macho ya wafuatiliaji wa muziki wa Bongo Fleva Tanzania
https://youtu.be/j5f-61WZ3mk

 

Lonely - Marioo

Lonely ya Marioo haijawahi kuchuja tangu kuachiwa kwake na ndio maana mashabiki wameendelea kuifuatilia kwenye mitandaoni. Video ya wimbo huu imeongozwa na Director Kenny.Utaniua - Zuchu

Utaniua ya Zuchu ni moja kati ya ngoma pendwa kwa sasa hasa video ya wimbo huo ambayo pia Diamond Platnumz anaonekana.Leave your comment