Mfahamu RJ The Dj Kutoka Tanzania

[Source: RJ The DJ]

Pakua Mixes Kali Za Rj The Dj Ndani Ya Mdundo 

Romeo George, ambaye anajulikana kitaalamu kama "RJ The DJ", amekuwa akiwaburudisha watu kwa takriban miongo miwili. Alifungua rasmi kazi yake katika tasnia ya burudani mwaka wa 2008 kama mtangazaji wa Redio na Televisheni ya Clouds Media, ambayo ni mojawapo kati ya vyombo vya habari vikubwa na maarufu sana nchini Tanzania.

Alizaliwa tarehe 16 Agosti 1988, Romeo alianza kufuata ndoto yake ya kuwa mwanahabari akiwa bado kijana. Alikuwa na hamu ya kupanua kazi yake ifike sekta nyingine za tasnia ya burudani. Wakati wake wa ziada, Romeo alijitolea kufuatilia kazi za wasanii waliobobea na hivyo kujifunza mengi sana kutoka kwa wasanii hao. Kando na hamu yake ya kuelewa usanii na burudani kwa undani, alizidisha bidii pia kujifunza taaluma ya 'Deejaying' na jinsi ya kutumia mashini za kisasa katika utumbuizaji


Mapenzi ya RJ kwa Deejaying na kuwaburudisha watu yamemfanya kuwa moja kati ya wasanii wanaoheshimika mno. RJ ni DJ Rasmi wa Diamond Platnumz, mmoja kati ta wasanii wakubwa sana Afrika. Ameburudisha pamoja na Diamond ulimwenguni kote katika nchi mbalimbali barani Afrika, na hata pia Ulaya. 

RJ pia kibinsafis ameweza kuburudisha katika maonyesho mbali mbali haswaa kwenye vilabu, uwanja wa michezo na viwanja vingine. Ujuzi wake umemwezesha kupata wafuasi sugu wanaomshabikia kwenye mtandao na pia anapoburidisha mbashara. Romeo anaamini katika kujituma na ana nia ya kuwa miongoni mwa Ma DJ bora duniani. Ameshinda tuzo nyingi ikiwemo "Best DJ" kwenye Tuzo za Muziki za Bongo, Tuzo za AEA USA, Tuzo za EAEA na kadhalika.

RJ ametimiza hatua muhimu kwenye taaluma ya 'Deejaying' kutokana na mafanikio yake kwenye ulingo wa huo ndani na nje ya Tanzania. Kando na kufanya Deejaying, RJ pia amefanya uigizaji. Amecheza nafasi mbali mbali kwenye vipindi ya televishenii. Moja kati ya uhusika uliopata mafanikio makubwa ni ule wa "Bill Junior", kwenye kupindi cha "Jua Kali". Romeo daima amekuwa na moyo wa kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii. Anavutiwa hasa na kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo, wanawake na watoto wasiojiweza kupata chakula na mahitaji mengine. Ni kwa sababu hii ndiyo alianzisha kampuni inayoitwa Jamii Moja

Leave your comment