Muziki Awards: Zuchu Aandika Historia Mpya Tanzania


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

Siku ya Jumamosi, kiwanda cha muziki Tanzania kilizizima na hii ni kutokana na tuzo za muziki Tanzania maarufu kama Tanzania Music Awards kufanyika siku hiyo na msanii Zuchu kuandika historia mpya kwenye tuzo hizo. 

Tuzo hizo ambazo huandaliwa na Baraza La Sanaa Tanzania maarufu kama BASATA zilirindima pale Superdom Centre Masaki, Dar Es Salaam ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo kufanyika baada ya kusitishwa kufanyika tangu 2015. 

Katika tuzo za mwaka huu, Zuhura Othman Soud yaani Zuchu aliibuka kidedea baada ya kubeba tuzo tano ambazo ni msanii bora wa kike, msanii bora wa kike Bongo Fleva, Video bora ya mwaka, Wimbo bora wa Bongo Fleva na Msanii bora wa kike chaguo la watu kidigitali. 

Kwa rekodi hiyo, Zuchu anakuwa msanii wa kwanza wa kike Tanzania kushinda tuzo tano kwenye tuzo za Tanzania Music Awards ndani ya usiku mmoja. 

Ikumbukwe kuwa Diamond Platnumz ndiye msanii anayeongoza kwa kushinda tuzo nyingi zaidi ndani ya usiku mmoja kwenye tuzo hizo baada ya mwaka 2014 kujinyakulia tuzo 7. Wasanii wengine ni 20% pamoja na Ali Kiba ambao walishinda tuzo tano.

Leave your comment