Darassa 'Dead Zone' Na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii
27 February 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Wakati tunaelekea kuumaliza mwezi Februari, wasanii kutoka Tanzania wameendelea kugawa dozi kali ya burudani kwa mashabiki zao kwa kutoa ngoma kali sana ambazo kwa, namna moja au nyingine zimefanya kiwanda cha burudani Tanzania kichangamke sana.
Kutoka kwa wasanii kama Darassa, Rayvanny, Kusah na wengineo wengi kutoka Tanzania, zifuatazo ni ngoma mpya kutoka Tanzania ndani ya wiki hii :
Dead Zone - Darassa
Baada ya ukimya wa takriban mwaka mmoja Darassa amerudi tena na Dead Zone, ngoma ambayo imesukwa na mdundo kutoka kwa T Touch ambapo ndani yake anatoa onyo na angalizo kwa watu wasiompenda.
Wasi Wasi - Kusah
Kama ulikuwa unasubiri ujio mpya wa Kusah, basi ondoa shaka kwani wiki hii Kusah alirudi na Wasi Wasi.
Kwenye Wasi Wasi Kusah anaturudisha kwenye muziki wa Zilipendwa kuanzia kwenye beat mpaka kwenye video na kupitia ngoma hii Kusah amedhihirisha namna ambavyo anaweza kubadilisha mtindo wake wa muziki.
Nobody - Darassa Ft Bien
Ili kutengeneza ngoma nzuri ya mapenzi, Darassa aliungana na Bien kutokea Kenya kutuletea Nobody. Humu ndani Darassa na Bien wanaimba kuhusu mapenzi na kupitia ngoma hii kwa mara nyingine tena Darassa anafanya kazi na msanii kutokea Kenya baada ya kushirikiana na Jovial.
Machozi - Stamina Shorwebwenzi
Kwenye Machozi Stamina anaugulia maumivu baada ya mkewe kumhadaa na kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao. Utapenda hadithi nzuri iliyopo kwenye ngoma hii pamoja na lugha ya sanaa aliyotumia Stamina kufikisha ujumbe wake.
Maan Meri Jaan - King & Rayvanny
Baada ya kutamba na Bongo Fleva, Kazomba, Amapiano na R&B, Rayvanny anashirikiana na King kutuletea Maan Meri Jaan, ngoma yenye vionjo vya kihindi ambayo imepokelewa vyema sana na mashabiki wa muziki.
Leave your comment