Jay Melody Adokeza Ujio Wa Ngoma Mpya Na Mejja

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli kutoka nchini Tanzania, Jay Melody hivi karibuni amedokeza kuhusu ujio wa collabo yake na rapa nguli kutoka Kenya, Mejja.

Jay Melody ambaye alianza safari yake ya muziki pale THT yaani Tanzania House Of Talent  amedokeza kuhusu ujio wa collabo hiyo hivi karibuni ikiwa ni miezi michache tu tangu aburudishe mashabiki zake na ngoma yake ya Nitasema ambayo kwa sasa inafanya vizuri sana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jay Melody alichapisha video inayomuonesha akiwa sehemu inayodhaniwa ni “location” ya video ambapo wawili hao yaani Jay Melody na Mejja  wanaonekana wakiwa wanacheza.

 Jay Melody aliambatanisha video na ujumbe uliosema “I Think You Are Not Ready” akiwa na maana kwamba “Sidhani kama mko tayari”

Kufikia sasa bado Jay Melody hajatangaza jina la ngoma hiyo wala tarehe anayotarajia kuachia mkwaju huo na bila shaka mashabiki kwa hamu zote wanasubiri sana ngoma hii.

 

Leave your comment