Jinsi Mtandao Wa Tik Tok Ulivyokuza Na Kuinua Muziki Wa Jay Melody

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Vanilla Ndani Ya Mdundo

Kwa mwaka 2022 Jay Melody alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri zaidi ambapo kupitia ngoma zake kama Sugar na Nakupenda ambapo mhitimu huyo wa Tanzania House Of Talent (THT) aliweza kuipeperusha vyema bendera ya muziki huu wa Bongo Fleva.

Ukiweka kando sauti yake maridadi na uandishi wake uliotukuka, kwa kipindi cha hivi karibuni, siri ya Jay Melody kutamba na kutawala vyema mbuga ya Bongo Fleva na hii pia inatokana pia na ngoma zake kupendwa kwenye  mtandao wa Tiktok.

Tiktok ni app ambayo ilianzishwa mwaka 2016 ikiwa inamilikiwa na kampuni ya Byte Dance na kwa sasa ni moja kati ya Apps maarufu sana duniani ikiwa na watumiaji zaidi ya Bilioni 1 kwa sasa.

Kama wasanii wengine wengi duniani, Jay Melody pia ni moja ya wasanii waliojiunga kwenye mtandao huo ambapo kufikia sasa ana wafuasi takriban 400k kwenye mtandao huo huku akiwa na likes zaidi ya Milioni 10.

Ngoma yake ya Nakupenda ya mwaka 2022 imetumika kwenye video zaidi ya Laki 9 huku hashtag ya Jay Melody Nakupenda ikiwa tayari imekusanya Hashtags Milioni 22. Aidha ngoma yake ya Huba Hulu pia imekusanya Hashtags zaidi ya Milioni 5 kwenye mtandao huo wa Tiktok.

Kwa msanii ambaye ni huru, hana usimamizi wa lebo kubwa, Tiktok bila shaka imekuwa ni msaada mkubwa sana kwa Jay Melody kwani watu wengi wamekuwa wakitumia ngoma zake kutengeneza video za Tiktok na kumfanya awe mkubwa zaidi.

Je Mtandao Wa Tiktok Umebadilisha Vipi Muziki Wa Jay Melody?

Jay Melody ni moja ya wasanii ambao wana pendwa sana na wasichana. Kwenye video mbalimbali hasa kwenye ngoma yake ya Nakupenda mabinti wengi walionekana kupagawishwa zaidi na wimbo huo na hivyo kutengenezea video za Tiktok. Pengine ni mashahiri yake, midondoko au sauti ya Jay Melody  ndio huvutia sana mabinti lakini bila shaka Tiktok imemsaidia sana Jay Melody kuvuna na kuwaleta karibu mabinti wa kike kwenye muziki wake,

Tiktok imechagiza watu wengi maarufu Tanzania kama wanamuziki, waigizaji na hata wachekeshaji kupendelea kutumia nyimbo zake kurekodi video za Tiktok Carpoza, Paula Kajala na wengineo wengi.

Kupitia ukuaji huu wa haraka Jay Melody amepata changamoto ya kuendelea kugusa hisia za shabiki wake kwa kuachia kazi mpya mara kwa mara na tarajio la kuafikia matakwa ya shabiki zake. Hii pia ikiwa kwenye nyimbo anazoshirikishwa.

https://www.youtube.com/watch?v=oKYMvnKR4M4

Leave your comment