Nyimbo Mpya: Ben Pol 'Wewe', Jay Melody 'Nitasema' na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ni wiki nyingine tena ambayo wasanii kutoka Tanzania wameamua kupamba kiwanda cha Bongo Fleva kwa kuachia ngoma kali ambazo zina lengo la kuwaburudisha mashabiki.

Kutoka kwa wasanii kama Jay Melody, Meja Kunta, Ben Pol na wengineo wengi zifuatazo ni ngoma mpya Tanzania kwa wiki hii :

Nitasema - Jay Melody

Baada ya Acha Wivu, Jay Melody ameleta ngoma mpya ya kuitwa Nitasema kwa mashabiki zake. Hii ni ngoma ambayo Jay Melody anatumia mahadhi ya Bongo Fleva ambapo anamuhakikishia mpenzi wake kuwa hatamuacha na kwamba siku zote ataendelea kusema anampenda.

https://www.youtube.com/watch?v=oKYMvnKR4M4

Mchepuko - Seneta Kilaka

Unakosa mengi kama bado hujaisikiliza Mchepuko ya Seneta Kilaka. Hii ni ngoma ya Singeli ambayo ndani yake Seneta anazungumzia kuhusu michepuko huku akiwa amegusia kuhusu tabia za michepuko na namna ambavyo anatamani yeye pia awe Mchepuko.

https://www.youtube.com/watch?v=n01ZFki9FCk

Ni Wewe - Ben Pol

Benpol anajulikana kwa uwezo wake wa kuandika ngoma za mapenzi na kwenye Ni Wewe Ben Pol amedhihirisha hilo kwani kupitia ngoma hii, mshindi huyo wa tuzo za Tanzania Music Awards anahadithia namna ambavyo anapata maumivu kutokana na kushindwa kumsahau mpenzi wake wa zamani

https://www.youtube.com/watch?v=1PtDJMuMWfA

Ruqaiya - Meja Kunta

Bendera ya muziki wa Singeli wiki hii ilipeperushwa vyema na Meja Kunta ambaye ameachia Ruqaiya ngoma nzuri ya mapenzi ambayo inatukumbusha ngoma za zamani za Meja Kunta kama Mamu, Naumia Na Moyo, Shory na nyinginezo nyingi.

https://www.youtube.com/watch?v=0QBZikuOBfA

Vavayo - Whozu Ft Marioo

Ili kutengeneza Vavayo, Whozu aliamua kuunganIsha nguvu na Marioo na bila shaka collabo hii imekosha sana hisia za mashabiki tangu ilipoachiwa kutokana na kuundwa na beat zuri la Amapiano pamoja na ujumbe mzuri wenye lengo la kutoa faraja

https://www.youtube.com/watch?v=TtT_xt3cJ0c

Leave your comment