Jay Melody Aachia Ngoma Mpya "Nitasema"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii nguli kutoka nchini Tanzania Jay Melody kwa mara nyingine ameamua kukata kiu ya burudani ya mashabiki zake baada ya kuachia mkwaju wake mpya kabisa unaoitwa "Nitasema".

Jay Melody ambaye pia alihusika katika uandishi wa ngoma ya "Ninogeshe" ya Nandy ameachia ngoma hii ya Nitasema ikiwa ni ngoma yake ya kwanza kwa mwaka 2023. Kabla ya Nitasema, Jay Melody aliachia Acha Wivu, ngoma ambayo ilipata mapokeo mazuri pia.

Nitasema ni ngoma ya mapenzi ambayo Jay Melody anatumia mahadhi ya Bongo Fleva kufikisha ujumbe wake. Ndani ya wimbo huu Jay Melody anakiri kuzama mzima mzima kwenye mapenzi huku akiweka wazi kuwa katika dunia hii anampenda mtu mmoja tu ambaye ni mpenzi wake.

Nitasema imetayarishwa na Genius Jini huku maandalizi ya mwisho ya wimbo huu yaani mixing and mastering ikiwa imeshughulikiwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records.

https://www.youtube.com/watch?v=oKYMvnKR4M4

Leave your comment