Uchambuzi Wa EP Mpya ya Mbosso Khan

Photo Credits: Twitter @mbossokhan

Downoad FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Sik kadhaa zimepita tangu mwanamuziki kutokea lebo ya WCB Mbosso atetemeshe kiwanda cha Bongo Fleva na EP yake ya mpya ya kuitwa Khan, EP ambayo imepokelewa kwa mikono miwili na mashabiki wa, muziki kutokea Tanzania. 

Khan EP ni mradi ambao Mbosso ametumia vionjo mbalimbali vya kimuziki kama Amapiano, Afrobeats pamoja na Bongo Fleva huku pia akiwa ameshirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo CEO wa WCB Diamond Platnumz, mwanadada Ruby, Mohamed Almanji, Costa Titch pamoja na Alfa Kat. 

Hizi hapa ni ngoma zote ambazo zinapatikana kwenye Khan EP ya kwake Mbosso. 

Huyu Hapa 

Mbosso anafungua Khan EP na "Huyu Hapa", ngoma ambayo imeundwa na vionjo vya Bongo na ambayo ndani yake Mbosso anaeleza ni kwa namna gani amezama kwenye huba zito na mpenzi wake. Mbosso alifanya uamuzi sahihi kuianzisha ngoma hii kwani inatukumbusha ngoma zake za zamani kama Hodari pamoja na Nadekezwa. 

Pole Featuring Ruby 

Ukiweka kando uandishi mzuri wa Mbosso kwenye ngoma hii basi pia utafurahia sauti ya kimamlaka na ya kubembeleza ya mwanadada Ruby. Kwenye ngoma hii Ruby na Mbosso wanatoa pole kwa watu wasiopenda penzi lao na ngoma hii inaendeleza dhima nzima ya mapenzi ambayo ndio kama lengo la EP hii. 

Shetani Featuring Costa Titch & Alfa Kat 

Mara nyingi Amapiano huwa ni muziki ambao utamu wake unapatikana kwenye beat zaidi kuliko kwenye mashahiri na kwa kulifahamu hilo, Mbosso kwenye Shetani anabadilisha mfumo kwa kutengeneza Amapiano ambayo ina mdundo mkali lakini pia ina mashahiri mazuri na yanayoeleweka. 

Uzuri wa ngoma hii unachagizwa pia na kiitikio chake ambacho kinashawishi mtu kuimba pamoja na mdundo mkali kutoka kwa S2kizzy. 

Wayo Featuring Ya Levis

Huu ni wimbo mwingine mzuri wa mapenzi katika EP hii ya Mbosso. Ndani yake Mbosso amemshirikisha msanii Ya Levis kutokea nchini Congo. Zaidi ya kuonesha kuwa ameshikwa vilivyo na mahaba, kwenye ngoma hii, Mbosso hana maneno mengi ya kusema na ni kwa kupitia ngoma hii kwa mara ya kwanza utamsikianosso akiimba kwa kutumia lugha ya kifaransa. 

Assaalam Featuring Mohamed Alamanji 

Watanzania wengi walikuwa hawamfahamu Mohamed Almanji kabla ya ngoma hii na bila shaka Assaalam ni mkwaju ambao umetimiza ndoto ya Mbosso ya siku zote kutaka kufanya collabo na msanii kutokea Uarabuni. 
Hii ni ngoma kwenye EP imeandikwa kwa ustadi mkubwa sana. 

Yataniua Featuring Diamond Platnumz 

Mkwaju huu ni mchanganyiko wa Afrobeats pamoja na Amapiano na tangu kuachiwa kwake wengi wameikosoa kwa kuchukua vionjo ya vya ngoma ya Asake Ya Peace Be Unto You pamoja na Adiwele ya Young Stanna. 
Ngoma hii  bila shaka itakuwa ni maarufu kwenye klabu na kumbi mbalimbali za starehe. 

Leave your comment