Wasifu wa DJ Summer Tz ,show zake kubwa na mziki wake
20 April 2022
[Picha: Dj Summer Instagram]
Free Download: Pakua Mixes kali ndani ya Mdundo
Immanuel John, almaarufu Dj Summer TZ alizaliwa tarehe 31 Desemba mwaka 1985. DJ Summer alianza rasmi kazi yake ya kuDJ mwaka wa 2005 katika mji wa Arusha, Tanzania. Hivyo, anajivunia kuwa na tajriba ya zaidi ya miaka kumi na mitano katika kazi hii. DJ Summer anatambulika kwa kucheza kwenye vilabu tofauti tofauti Tanzania. Kwa sasa, ni mmoja wa madj tajika nchini Tanzania na eneo la Afrika Mashariki.
Kando na kucheza kwenye vilabu, DJ Summer TZ pia amebarikiwa kufanya kazi na stesheni kadhaa za redio. Kwenye miaka kumi na tano aliokuwa kwenye kazi hii, DJ Summer amebahatika kufanya kazi na MJ Radio (Arusha), Kiss FM (Mwanza) na East Africa TV and East Africa Radio 2012 ambapo ndipo anafanya kazi sasa.
Tuzo Alizoshinda
STR8 Music DJ Competition 2010-2011
Show zake kubwa ni kama gani?
Planet Bongo
Yeyote anayetaka kumskiza DJ Summer anaweza mpata hewani siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kwenye show ya Planet Bongo masaa ya saa saba hadi saa kumi mchana. Show hii ni ya muziki wa Bongo pekee.
The Cruise
Pia unaweza mskiza DJ Summer kwenye show ya The Cruise siku ya Jumatatu hadi Alhamsi majira ya saa tatu hadi saa sita mchana.
Top Playlist
Show hii iko siku ya Jumapili kuanzika saa nne hadi saa nane mchana. Kwenye show hii, DJ Summer anacheza mchanganyiko wa muziki mpya pekee.
Friday Night Live
Show hii iko siku ya Ijumaa kuanzia saa saa tatu hadi saa tano usiku. Show hii hupeperushwa moja moja kwenye stesheni ya TV.
Leave your comment