Mfahamu DJ Feruuh, Mixes zake za Taarab na Show zake kubwa

[Picha: Dj Feruuh Instagram]

Free Download: Pakua Mixes kali ndani ya Mdundo

DJ Feruuh ni nani?

Jina la usani: DJ Feruuh

Jina halisi:   Ally Mussa Maulid

Mix tapes zake ni za muziki gani: Taarab

DJ Feruuh alianzaje kazi yake ya kuwa DJ na lini?

Ally Mussa Maulid maarufu kama DJ Feruuh alianza rasmi kazi yake ya  kuDJ mwaka wa 2009 kule Zanzibar, Tanzania. Hivyo, anajivunia kuwa na tajriba ya zaidi ya miaka kumi na mitatu katika kazi hii.

DJ Feruuh anatambulika kwa kucheza kwenye vilabu tofauti tofauti nchini Tanzania. Kwa sasa, ni mmoja wa madj tajika nchini Tanzania na eneo la Afrika Mashariki.

Kando na kucheza kwenye vilabu, DJ Feruuh pia amebarikiwa kufanya kazi na stesheni kadhaa za redio na televisheni . Kwenye miaka kumi na miwili aliokuwa kwenye kazi hii, DJ Feruuh amebahatika kufanya kazi na Breeze FM (Tanga), Coconut FM (Zanzibar) na Choice FM ( Dar es Salaam)

Mwaka wa 2015, alijiunga na Clouds FM na Clouds TV ambapo anafanya kazi hadi sasa.

Mixes Za Taarab

Katika kucheza mziki kama DJ, Feruuh anaumaarufu mkubwa ndani ya mtamdao wa mdundo kwa kuwa na mixes kali za mziki aina ya taarab, Qaswida na hata bongo mixes.

Akishikiana na kampuni ya mziki Mdundo.com Dj Feruuh hutengeza mixtapes au mixes kali za taarab. Mwaka huu Feruuh anajhusiki vile vile kwenye shughuli nzima ya Dj Battle na waeza kipakua mixes zake hapa.

Show zake kubwa ni kama gani?

  • Leo Tena 
  • Trafik Jams
  • Amplifaya na Millard Ayo 

Amefanya Kazi wa Wasanii gani?

DJ Feruuh ndiye DJ rasmi wa mkurugenzi mkuu wa Kings Music Alikiba.

Ngoma Zake Bora ni Kama Gani?

Kando na kucheza santuri, DJ Ferruh pia huachia nyimbo zake akiwashirikisha wasanii tajika kutoka Bongo. Nyimbo zake bora ni kama vile:

  • Saula ft Mabantu 
  • Ukisimama ft B2K 
  • Sawa ft M.M.S 
  • Kinai  ft Feisal

Show Zake Kubwa ni Kama Gani?

  • Kila wiki DJ Feruuh hucheza santuri kwenye clouds TV siku ya Jumatatu hadi Ijumaa. Kwenye show hii, yeye hucheza muziki zote.
  • Siku ya Ijumaa, DJ Feruuh ana kipindi kiitwacho ‘Wazee na Mbanga’ kwenye Clouds TV. Show hii inaanza saa tisa jioni hadi saa kumi na moja. 

 

Leave your comment