Nimefika Hapo.

Muziki ninauheshimu sana.
Tuseme, nilianza kupenda muziki ningali mdogo.
Nakumbuka wasaani pale mitaani nilipokulia, wengi waliingia kwenye usaani, baadaye Maisha yakawa hivyo, na wakasare hizo. Nakumbuka, hawakuwahi kuchukuliwa serious kwa hiyo direction walichukua.
Mimi nilipenda masomo, japokuwa nilikuwa naandika songs pia. Sikuwa huyo msaani mwenye Wangesifia hapo mitaani, lakini chini ya maji wengi waligundua ninaweza sana. Japo sikuwa MTU wa kuonyesha wazi wazi.
Kwa namna hiyo, ndivyo nilivyoweza kurekodi wimbo wangu Wa kwanza nikiwa mwaka wa kwanza Chuoni kikuu, na hakuna aliyegundua sana maana sikuwahi kuweka wazi wazi. Hadi sasa, hiyo ndiyo hulka yangu. Bado sijawahipata hamu ya kushusha utamu Wa mziki ili niende mainstream.
Kwa njia hiyo, imenibidi, nijifunze kufurahia kutengeza mziki tu. Sina mengi. Asante kwa wale hunisikiliza ninapotoa nyimbo Mara kwa Mara. Bado Niko mzima. Nitaakikisha mnapokea utunzi wangu wakati wowote Nina capital ya kufanya hivo . Msisahau, bado nimeokoka, nampenda yesu.- Tony Bigmile, Wa Tony Bigmile Music.

Leave your comment