Ommy Dimpoz Adhibitisha Ujio wa Kolabo Baina Yake na Marioo

[Picha: Ommy Dimpoz]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Ommy Dimpoz amedhibitisha ujio wa kolabo baina yake na msanii Marioo. Ommy Dimpoz aliwaonjesha mashabiki wake kionjo cha wimbo huo ambao upo katika mtindo wa Swahili Amapiano.

Ommy Dimpoz hakufichua habari zaidi kuhusu ngoma hiyo na hivyo basi mashabiki wamebaki na hamu sana kuuskiza.

Bado haijafahamika iwapo ngoma hiyo ipo kwenye albamu ya Ommy Dimpoz ambayo inatarajiwa kutoka wakati wowote toka sasa, ama ni ngoma tu ambayo itaachiwa kivyake.

Ommy kwenye mahojiano ya hivi karibuni na Wasafi FM, alidokeza kuwa huenda akaachia kazi mpya kabla ya mwaka huu kuisha japo zimesalia siku chache.

"Nilikuwa narekodi albamu, na kama unavyoona kwenye background Fally Ipupa nmefanya naye yupo. Kwa hiyo maybe kunaweza kukawa na surprise ya kufungia mwaka. Mwaka mwenyewe umebakiza siku ngapi, so anything can happen," ndio yalikuwa maneno ya Ommy Dimpoz alipoulizwa iwapo bado ataachia kazi yoyote mwaka huu.

Ifahamike kuwa Marioo sio mgeni kwenye mtindo huu na ni sahihi kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya waanzilishi wa muziki wa Swahili Amapiano.

Mtindo huu unaunganisha mtindo mbili ambayo ni bongo kutoka nchini Tanzania na Amapiano kutoka Afrika Kusini. Baadhi ya ngoma za Swahili Amapiano kutoka kwa Marioo ambazo zimefanya vizuri sana ni pamoja na 'Beer Tamu' na 'Mama Amina' ambayo aliwashirikisha Sho Madjozi na Bontle Mouth.

 

Leave your comment