259 EP

Msanii wa Hip-Hop/Rap kutoka Mwanza, Tanzania ameachia EP yake mpya iitwayo “259” iliyotoka rasmi tarehe 25 mwezi wa 9. EP hiyo ina jumla ya nyimbo 6 na inapatikana kwa mfumo wa soft copy kwa njia ya WhatsApp, Email au Telegram. Project hiyo bado haijawekwa katika digital platforms zozote zile mpaka pale zitakapotoka taarifa zaidi:

Katika EP hiyo Fivara amechana kwenye midundo ya Wadundishaji tofauti tofauti akiwemo Offstress Beatz, Odilla Beatz, kILLy na Aby Bangladesh. Naweza kusema hii ni EP kali kabisa kwa mwaka huu kutokana na utengenezwaji wake kuanzia midundo, uchanganyaji wa sauti na umaliziaji. Kazi kubwa imefanyika kwenye uandishi na pia Wavoko kutoka B.I.G records kafanya kazi nzuri kwenye mixing na mastering.

Kuipata EP hii lipia Tshs 5,000 kupitia M-Pesa namba 0769 477 219 au Airtel money namba 0692 922 497 na jina likiwa ni Jordan Wilson Zabron kwa namba zote mbili. Baada ya kufanya muamala tuma au hakikisha taarifa za muamala wako na utatumiwa soft copy yako.

Jina la mradi: 259 EP.
Msanii: Fivara.
Producers: Offstress Beatz, Odilla Beatz, kILLy & Aby Bangladesh.
Mixing & Mastering: Wavoko.
Studio: B.I.G Records.
Label: Pie Muzik.
Mwaka: 2021.

Leave your comment