Harmonize Alazimika Kusitisha Sehemu ya Ziara yake Ulaya

[Picha: Capital FM]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Harmonize ametangaza kusitishwa kwa sehemu ya ziara yake ya muziki Ulaya. Kwa sasa, Harmonize yuko Marekani ambako anaendelea na ziara yake ya muziki inayotarajiwa kudumu kwa miezi miwili.

Soma Pia: Cheed Atangaza Tarehe Atakayoachia Ngoma Yake Ya Kwanza Chini Ya Konde Music Worldwide

Harmonize hata hivyo ameomba mashabiki wake radhi kwani hataweza kutumbuiza katika baadhi ya mikoa ambayo alikuwa ameorodhesha kwenye ziara yake hapo awali.

Kwa mujibu wa tangazo la Harmonize, ziara yake imesitishwa katika sehemu za nchi ya Kanada na Uswidi, kutokana na hatua ambazo serikali za mataifa hayo yamechukua dhidi ya kusambaa kwa maambukizi ya COVID-19.

Harmonize alichapisha ratiba mpya ya ziara yake ya tarehe na mikoa atakayotumbuiza.

Soma Pia: Meneja wa Harmonize Ajibu Wakosoaji Wanaomsema Msanii Huyo Vibaya

Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide aliwaahidi mashabiki wake watakaohudhuria tamasha yake burudani isiyo na kifani.

"Blood people in Canada & Sweden  so sorry to tell you that I’m not going to make it for our current schedule date do to covid-19 restrictions so I will update all my beautiful loyal fans asap on the new tour dates to everybody who got the ticket ready trust me I will be there in God's plan  inshallah so yeeeeessss promotas in USA it's now time ...!!! Let's fill up the available dates check with my guy @dj.Storm6 let's go Las Vegas 24/9/ New York 1/10/ LA 9/10/ Boise Idaho 15/10 Minnesota 22/10 and more," chapisho la Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram lilisomeka.

Leave your comment