Bob Junior Aeleza Alivyotengeneza ‘Itetemeshe’ Akimshirikisha Lava lava

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kwa sasa, wimbo wa Bob Junior akimshirikisha Lava lava ‘Itetemeshe’ ni mojawapo ya nyimbo ambazo zinazosumbua sana kwenye redio na TV nchini Tanzania.

Akiongea kwenye kipindi cha The Switch, Bob Junior ameeleza kuwa alipata wazo la wimbo huo baada ya kusikilizishwa mdundo wa nyimbo hiyo na mtayarishaji muziki Halonen na baada ya kupendezwa na beat la wimbo huo, ndipo akaanza kuandika mistari.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mbili ‘Your Love’ na ‘Tulizana’

"Nilikuwa nimeenda kuonekana na Halonen producer kufika pale akaniekea midundo alipoiweka hiyo beat nikasema eeh mbona kali em tujaribu kufanya kitu then tukakaa tukatafuta ideas na nikarecord," alisema Bob Junior.

Aidha, Junior alidokeza kuwa baada ya msanii Lava lava kusikia demo ya wimbo huo, alivutiwa nayo na siku hiyo hiyo Lava lava alirekodi kipande chake cha wimbo.

"Nilikuwa na demo ya hiyo nyimbo akaisikiliza (Lava lava) akaniambia daah mwanangu Bob mbona kali sana kama bipi acha nijae humo… Huwezi kuamini Lava lava siku hiyo alivyoisikiliza tukaenda tukarekodi ngoma ikawa kali," alidokeza Bob Junior.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mbili ‘Your Love’ na ‘Tulizana’

 Bob Junior ni Nani?

Bob Junior ni mwanamuziki na pia ni mtayarishaji nguli wa muziki hapa nchini Tanzania. Kwenye upande wa kuimba Junior ametoa ngoma nyingi ambazo zimefanya vizuri miaka kadhaa nyuma kama ‘Nichum’, ‘Nanini’ na ‘Oyoyo’.

Kwenye upande wa utayarishaji muziki, Junior anakumbukwa kwa kutayarisha ngoma ambazo zimemtoa Diamond Platnumz kimuziki kama ‘Kamwambie’, ‘Mbagala’ na ‘Ntarejea’.

Ngoma yake ya ‘Itetemeshe’ ni ujio wake mpya kwenye kiwanda cha muziki na bila shaka imepokelewa vizuri sana na mashabiki.

Leave your comment