Chidi Benz Amkumbuka Vanessa Mdee katika sanaa Kwa Ujumbe Mzito

[Picha: Chidi Benz Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bila shaka tunaweza kusema kuwa msanii Chidi Benz ameona pengo la mwanadada Vanessa Mdee kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kuweka chapisho kwenye akaunti yake instagram linalomuhusu Vanessa Mdee.

Chidi Benz ambaye amekua  kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa muda mrefu sasa, alichapisha picha ya Vanessa Mdee na kuisindikiza na ujumbe, "Sema Tanzania nayo from nowhere tumefanya my sis Vanessa Mdee kuuchukia muziki, ilikuwa tunahitaji sana vitu kutoka sauti Ile. Sijui wengineo,” aliandika.

Haijajulikana bado ni kwanini Chidi Benz ameandika ujumbe huo mzito kuonyesha masikitiko yake juu ya uamuzi huo wa Vanessa, kwani wasanii hao wawili hawakuwahi kuonekana dhahiri kuwa na ukaribu au urafiki.

Soma Pia: Rosa Ree Awasihi Wasanii wa Bongo Kuacha Kufanya Kiki Katika Muziki.

Ujumbe huo kutoka kwa Chidi Benz unakuja ikiwa umeshatimia mwaka mmoja tangu Vanessa mdee atangaze kuacha muziki rasmi.  Mwezi Juni mwaka jana, Vanessa kupitia podikasti yake ya "Deep Dive With Vanesa Mdee” alisema ameamua kujiondoa katika tasnia ya muziki kwa kuwa tasnia hiyo imejaa mambo ya ajabu na yasioaminika machoni pa watu.

“Kilichonifanya nichukue likizo kwenye muziki ilikuwa ni kuchagua maisha yangu na muziki unajua unapoingia kwenye tasnia watu wanakuambia upande mmoja tu wa mazuri na kusahau mabaya, kiukweli tasnia ya muziki imejaa mabaya mengi na ilibidi nichague kundelea kwenye ubaya au maisha yangu" alisema Vanessa mdee.

Tangu Vanessa Mdee atoe taarifa hiyo msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Mdee Music hajatoa wimbo wowote na kwa sasa anaishi Atlanta nchini Marekani akiwa na mpenzi wake Rotimi ambaye ni mnigeria anayeishi Marekani.

Tangu aanze muziki rasmi 2013 Vanessa ameachia album moja inayoitwa "Money Mondays" ambayo imeshirikisha wasanii wakubwa kama Joh Makini, Mohombi, Radio & Weasel pamoja na Reekado Banks nchini Nigeria.

Leave your comment