Waah vs Attitude: Je ni Collabo Gani Bora ya Diamond ama Harmonize?
27 April 2021
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Wiki iliyopita, mwanamuziki tajika nchini Tanzania Harmonize aliaachia wimbo mpya kwa jina ‘Attitude’ akiwashirikisha Awilo Longomba na H Baba.
Wimbo huu ulizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, huku wapenzi wa muziki wakiilinganisha na wimbo wake Diamond Platnumz ‘Waah” aliyomshirikisha Koffi Olomide.
Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea Leo Usiku
Katika nakala hii, tunachambua nyimbo zote mbili huku tukiangazia uzuri wao:
Utazamaji
Baada ya Harmonize kuachia wimbo wa “Attitude”, ngoma hio iliweka rekodi mpya kuwa wimbo wa kwanza kupata zaidi ya watazamaji elfu mia moja kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzanai. Awali, rekodi hii ilikuwa ya Diamond Platnumz kwa wimbo “Waah” iliyopata utazamji huu ndani ya dakika 48.
Kuwashirisha Wasanii Tajika Kutoka Congo
Kwenye wimbo wake wa ‘Waah”, Diamond alimshirikisha Koffi Olomide, huku Harmonize akimshirikisha Awilo Longomba. Baada ya Harmonize kuachia wimbo wake, kuna wachache waliomkejeli wakidai kwamba anaiga vitu alivyofanya Diamond. Inaaminika kuwa uamuzi wa kuwashirikisha wasanii nguli kutoka Congo imeskuma nyimbo hizi kufanya vizuri kwani muziki wa Lingala na Rhumba unapendwa kote Afrika.
Video
Nyimbo zote mbili zina maudhui ya densi. Unapozisikiliza, kuna uwezwkano mkubwa kwamba utaamka na kusakata densi. Video zote mbili pia zina mdundo mzuri unaokupa raha unaposikiza ngoma hizi mbili.
Lugha
Katika wimbo wa ‘Waah’ Diamond ametumia lughya ya Kiswahili na anajieleza kwa njia ya kishairi. Ngoma hii imeandikwa vizuri na imekubalika Afrika mashariki ma nchi zingine zinazozungumza Kiswahili. Changamoto NI kuwa wasioelewa Kiswahiliwanaweza kosa kuelewa ule ujumbe jinsi unavyofaa. Kwingineko, Harmonize ametumia mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza ili kuwafikia wafuasi wake wote; wanaolewa Kiswahili na wasioelewa.
Leave your comment