Zuchu Ateuliwa Balozi wa Kampuni Kubwa Tanzania

[Photo Credit: Zuchu Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii kutoka lebo ya wasafi amesaini dili kubwa ya kuwa balozi wa kampuni moja ya vipodozi ijulikanayo kama Tridea cosmetics.

Dili hio ilitangazwa jana kupitia kwa Mtandao wa Instagram.

Kupata ubalozi huo ni dhihirisho kuwa Zuchu sasa ameanza kupata fanaka katika biashara yake.

Hivi karibuni baada ya kutambulishwa kama msanii katika lebo ya Wasafi, Zuchu alijifungulia biashara ya kufanya upodozi almaarufu Zuhuraty beauty and make up.

Hivyo basi ni dhahiri kuwa Zuchu ndiye mtu mzuri wa kuwasaidia kampuni hiyo ya Treadea cosmetics.

Soma Pia: Zuchu Drops New Song ‘Shangilia’

Msani yeyote anapoanza kupata ubalozi inaashiria kuwa kampuni hiyo inaamini umahiri wa Zuchu na kuwa atawapa hadhi katika biashara yao.

Zuchu kwa upande wake ni msanii wa tatu kutoka lebo ya Wasafi kupata Ubalozi huku, Mbosso akiendeleza ubalozi wa kapuni ya Maziwa ya Tanga Fresh na Diamond naye akiwa balozi wa Pepsi na Coral paints.

Kufikia sasa Zuchu amepata umaarufu mkubwa wa kuwa msanii wa kwanza wa kike kuwa na mashabiki wengi hasa kwenye mitandao ya kijamii na ya kucheza mziki kama YouTube.

Soma Pia: Zuchu’s ‘Nobody’ Hit Featuring Joeboy Ranked among Top 10 Songs in Africa

Kwingineko, mziki wake Zuchu unaendelea kupata umaarufu huku akiendelea kuachia mziki unaowafurahisha wengi. Hii leo Zuchu ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa mapenzi wake Rayvanny uitwao “Number One” huku video ya wimbo huo ikitarajiwa hivi karibuni.

Leave your comment