Nyimbo 5 Zilizovuma Bongo Wiki Hii [Video]

[Photo Credit: Alikiba Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Wasanii wengi nchini Tanzania wanaendelea kutoa nyimbo mpya kila kukicha.

Wiki hii, video kadhaa zimevuma mitandaoni na kupata kutazamwa na watu wengi.

Baadhi ya video zilizofanya vizuri ni:

Haunisumbui - Diamond Platnumz

“Haunisumbui” ni wimbo wake Diamond akisimulia hadithi ya mpenzi wake wa kitambo ambaye amekuwa akimsumbua kwa muda baada ya mapenzi yao kuvunjika. Kulingana na Diamond, yule wa zamani hapaswi kuingilia maisha yake tena, kwani yote anofanya kwa sasa hayamsumbui kamwe. Kwa sasa ni wimbo aina ya audio tu na umetazamwa zaidi ya mara laki nane.

https://www.youtube.com/watch?v=BgI4x51X8WU&ab_channel=DiamondPlatnumz

Mediocre - Alikiba

Huu ni wimbo wake Alikiba uliozua gumzo mitandaoni wengi wakitaka kujua ni nani wanaoangaziwa kwneye maneneo ya wimbo huu. Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kuchezwa na watu wengi huku wengine wakitumai watapata majibu yao. Kufikia sasa wimbo huu unawatazamji zaidi ya Millioni mbili nukta nne.

Download Alikiba Music for Free on Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=6Xbk4Qa-0co&ab_channel=KingsMusicRecords

Naanzaje – Dully Sykes na Maua Sama

Ni wimbo ambao Dully sykes amerejea nao kwenye ulingo wa muziki wa bongo. Wawili hawa wanelezea uzuri uliko kwenye mapenzi na jinzi ya kulinda penzi lao. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa zaidi ya mara lakini moja.

https://www.youtube.com/watch?v=ecXMrDoC8Pg&ab_channel=DullySykes

Litawachoma – Zuchu na Diamond

Wimbo huu umetazamwa zaidi ya mara milioni mbili kwenye YouTube chini ya wiki mbili. ‘Litawachoma’ ndio wimbo wa kwanza ambao Zuchu amemshirikisha mkuu wake Diamond Platnumz.

https://www.youtube.com/watch?v=g9spgkHS2bs

Cheche – Zuchu na Diamond

Video ya wimbo hii ni kati ya video zilifanya bora zaidi nchini Tanzania mwezi wa Septemba. Kati wimbo huu, Diamond na Zuchu wanadhihirisha mapenzi yao.

https://www.youtube.com/watch?v=vyUslddxOpI

 

Leave your comment