Diamond, Zuchu Wang’aa Kwenye Nyimbo Tano Bora Zaidi Mwezi September

[Photo Credit: Zuchu Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Wanamziki kutoka Tanzania wamefanya kazi nzuri mwezi huu wa September kwa kuachia nyimbo zilizowapendeza mashabiki wengi.

Kwenye nakala hii, tunaangalia nyimbo tano bora zaidi mwezi wa September:

Cheche - Zuchu na Diamond Platnumz

‘Cheche’ ni wimbo wa kwanza ambao Zuchu amemshirikisha mkuu wake Diamond Platnumz. Cheche ilipaata umaarufu kwa kuwa watu wengi walikuwa wanasubiri Wasafi records iachie wimbo unaowashirikisha wasanii hao wawili.Chini ya kipindi cha wiki mbili, wimbo huo umetazamwa zaidi ya mara milioni tatu kwe YouTube.

Download Diamond Music for Free on Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=vyUslddxOpI&ab_channel=Zuchu

Litawachoma - Zuchu na Diamond Platnumz

'Litawachoma' ni wimbo wa mapenzi ambapo Zuchu na Diamond wanaelezea mapenzi yao kwa kila mmoja na kuwachana wale wanaopinga hiyo. Wimbo huu ulizua gumzo kwenye mitandao kwa ubora wake huku video ikiwa ya kupendeza sana na picha za kimapenzi zinazoonyesha Diamond na Zuchu wakiwa na wakati mzuri kwenye seti. Kwa sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya Millioni moja nukta mbili siku mbili baada ya kuzinduliwa kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=g9spgkHS2bs&ab_channel=Zuchu

Mediocre - Alikiba

Kwenye ‘Mediocre’, Alikiba anazungumza juu ya msimamo wake katika tasnia ya muziki kwa miaka 18 iliyopita. Wimbo huu pia umezua gumzo mashabiki wakitaka kujua Alikiba alikua anazungumzia kina nani. Kufikia sasa ‘Mediocre’ ina watazamaji zaidi ya milioni moja nukta sita.

https://www.youtube.com/watch?v=6Xbk4Qa-0co&ab_channel=KingsMusicRecords

Ongeza - Diamond Platnumz

Wimbo huu unaleta mihemko ya siku ambazo Diamond alifanya muziki wa mapenzi. Katika wimbo wa "Ongeza" Diamond anasimulia maisha yake ya zamani ya mapenzi na jinsi yalivyokuwa mazuri. Walakini, sasa kwa kuwa hawapo pamoja tena, anahisi anachofanya ni kuongeza maumivu kwa machungu alonayo tayari. “Ongeza” ina zaidi ya watazamaji milioni moja nukta moja na video yake bado haijaachiliwa.

https://www.youtube.com/watch?v=-AX3WTAmJno&ab_channel=DiamondPlatnumz

Sina Nyota - Mbosso

'Sina Nyota' ni simulizi ya mtu aliyeumizwa na kuvunjika kwa kile alidhani ni mapenzi ya kweli. Mbosso anasimulia jinsi sasa ni mtu asiye na tumaini baada ya nyota yake kuacha kuangaza. Wimbo huu kwa una zaidi ya watazamaji milioni tatu.

https://www.youtube.com/watch?v=Bi2MXmKLZuQ&ab_channel=Mbosso

Leave your comment