Otile Brown Pens Emotional Letter to President Kenyatta Decrying Misappropriation of Artists’ Funds

[Photo Credit: Standard]

By Omondi Otieno

Follow Us on Google News

Celebrated Kenyan artiste Otile Brown has penned an emotional letter to President Uhuru Kenyatta calling for stringent measures against those misappropriating artists’ money.

In his letter, Otile noted that artists are struggling to earn a living, yet some CMO officials are squandering their money.

He urged the president to intervene on the issue and ensure that the artists earn what is due to them.

Here is Otile Brown’s Full Letter to the President as Posted on his Instagram Page:

I feel you’re pain my brother @willy.paul.msafi Hakika nimelia… Mheshimiwa Rais @ukenyatta heshima yako. Samahani! Nina machache ya kusema endapo yatakufikia.  Mimi ni msani Mzalendo wa mziki wa kizazi kipya toka hapa nchini nafahamika kama Otilebrown na kutokana na utafiti tunafahamu fika kua nchi hii yetu ya kenya ni nchi yenye changa moto za ukosefu wa ajira kwa vijana .Alhamdulilah! “ Wengine” tumejaaliwa vipaji vinavyotuwezesha kujipa kipato kidogo kupitia tasnia ya mziki , tumejitengenezea ajira bila usaidizi wowote wa Serikali na bado huwa tunalipa ushuru inavyostahili bila kulalama ...

Chakusikitisha nikua bado hatupati tunachostahili , viongozi na wasimamizi wanatupora nakutudhulumu wakati wengi wetu tumetoka kwenye familia za kimaskini na tunategemewa kiasi kikubwa... Swali langu ni wasimamizi wa MCSK baada ya kukiri na kukubali mashtaka, ni hatua gani watachukuliwa?? Tungependa kuona wamefungwa gerezani na mali zao kuchukuliwa na kurudishwa kwenye tasnia ya sanaa .. kama kweli tuna utu na tunataka mabadiliko kwenye nchi yetu..

Inauma sanaa mheshimiwa Rais @ukenyatta Sahii kwanzia January inasemekana kuwa serikali inataka kuanza kututoza ushuru kupita mtandao wa YouTube ambao tumekua tukitegemea baada ya kutukata tamaa na viongozi waliokataa kutupatia haki yetu na kutudhulumu hadharani. Bila woga. Nahisi umefika wakati wanatukatisha tamaa , tumetengwa na hakuna anayetujali hata kile kidogo cha kulisha familia zetu kinachukuliwa.

I love my country. Mwenyezi mungu tusimamie. Mheshimiwa Rais @ukenyatta .. we’re not asking for anything from the government but to be given, what is rightfully ours .. please please please

Leave your comment