TANZANIA: Roma na Stamina, Wamkana Lulu

Wasanii wa muziki wa HipHop wanaounda kundi la Rostam, Roma Mkatoliki na Stamina wamekanusha kumuimba msanii Lulu, maarufu Elizabeth Michael katika wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la "Kaolewa".

Wakizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, msanii Stamina amesema wimbo huo haujaelekezwa kwa mtu yoyote isipokuwa lengo lao ni kuonesha mwanamke mwenye tabia kama ya Mwajuma ndani ya jamii ya kitanzania.

"Hapana sisi hatuja muimba Lulu, Mwajuma ni mwanamke mtata, mcharuko, anajulikana mtaa mzima kwa vituko vyake,watu wakasema haolewi lakini mwisho wa siku ikatokea amefunga ndoa.sasa sidhani kama Lulu ana tabia hizo," amesema Stamina

Kwa upande wake Roma amesema walikuwa na wazo la kumchukua Wema Sepetu kama video queen wa video yao lakini mke wake aliwashauri kuwa asingeweza kufaa sababu hana tabia za uswahilini.

"Pia tulikua na wazo la kumchukua Wema Sepetu ila mke wangu akasema Wema hawezi fiti, ndio maana tukamchukua Nisha na amefanya kile ambacho sisi tulikua tunakitaka,japo wengi walijua Riyama ndio angekuwa Mwajuma. Wapo wengine ambao wangefaa hata Shilole sema ameshaolewa", amesema Roma.

Source: eatv.tv

Leave your comment