AZIMIO LA AMANI LA UTAMADUNI WA HIP-HOP

AZIMIO LA AMANI LA UTAMADUNI WA HIP HOP.

 Maazimio ya amani ya Hip hop yaliwasilishwa katika baraza la Umoja wa mataifa tarehe 16/05/2001.Na kutiwa sahihi na mashirika mbalimbali yaliwemo Temple of Hip Hop, Ribbons International, UNESCO na pia wanaharakati wa hiphop 3000, waasisi na pia washiriki wa Baraza la Umoja wa Mataifa. 

​Awali kabisa nyaraka hizo zinatambua utamaduni wa Hip Hop kama nyenzo mojawapo ya kulela amani na maendeleo. Ni mkusanyiko wa kanuni ambao unashauri au kuelekeza wanahiphop jinsi ya kutunza, kuthamini na kulinda hali ya amani kupitia utamaduni wa Hip Hop duniani kote.

 Mkakati huo ukaongeza zaidi kuwa utamaduni wa Hip Hop ni tanzu chanya na wala haina uhusiano na tanzu hasi ambazo huchochea vijana kuvunja sheria za nchi.KRS One, Pop Master Fabel, Afrika Bambataa, Ralph Mc Daniel na Harry Allen walikuwapo katika kuandaa maazimio hayo. 

Azimio la Amani la utamaduni wa Hip Hop.

 Azimio la utamaduni wa hip hip huongoza watu katika utamaduni wa uhuru na kuepuka vurugu au machafuko, na pia kutoa ushauri na  ulinzi katika kuendeleza utamaduni na jamii za watu wa Hip Hop kimataifa. Kupitia kanuni za azimio hili, Utamaduni wa Hip Hop umeanzisha msingi wa Afya, Upendo, Utambuzi, Mali/Utajiri, amani na maendeleo kwa ajili yetu watoto wetu wajukuu zetu daima milele. 

 Kwa ajili ya kupata maana na malengo ya Hip Hop, au kama mtu atahoji juu ya Hip Hop, au endapo wanahiphop watapata mtafaruku juu ya Hip Hop, basi watu hao hawana budi kurejea andiko la azimio hili. Watumie azimio hili kama mwongozo wao kwa ushauri na ulinzi wa tamaduni hii ya Hip Hop. 

Kanuni ya kwanza

 Hip Hop ni utamaduni unaoelezea au kufafanua uhuru wetu kwa pamoja na kujitambua kwetu ,tangu kukua kwake utamaduni huu uliwasilishwa  kupitia mavunjaji, uchenguaji, machata , umanju, midundo ya mdomo, Elimu ya mtaani na ujasiriamali. Kivyovyote na kokote vipengele au chembechembe hizi za utamaduni wa hiphop na zinazokuja huko mbele, Azimio hili la amani la utamaduni wa Hip Hop ni lazima lishauri matumizi ya vipengele hivi kuakisi maisha yetu ya kila siku. 

Kanuni ya Pili

 Utamaduni wa Hip Hop unaheshimu sana utu na thamani ya maisha ya kila mtu bila ubaguzi wowote.Wana hip hop ni lazima wazingatie ulinzi na maendeleo ya maisha kabla na baada ya mwanadamu kuamua kuangamiza, kuhatarisha au kutafuta maisha yake mwenyewe. 

 Kanuni ya tatu

 Utamaduni wa Hip Hop unaheshimu sheria pamoja ya makubaliano au mikataba ya utamaduni wake (Azimio lake), kuheshimu nchi yake, taasisi zake na yoyote anayefanya biashara na mwana Hip Hop basi hategemewi kuvunja sheria na makubaliano.

Kanuni ya nne


Hip Hop ni utamaduni unaoeleza kuhusu uhuru wetu na kujitambua kwetu, kujitambua katika Nyanja ya maisha, na kutambua umuhimu au ushawishi wetu katika jamii hasa hasa kwa watoto na milele tutaheshimu haki na ustawi.Utamaduni wa Hip Hop unahamasisha  ubinadamu na udugu kwa kina dada, kina mama, kina kaka kwa watoto na familia.Tunajitambua kutodhamiria kuleta madhara yoyote kwenye Jamii ambao yatahatarisha utu na sifa za watoto wetu, wakubwa zetu na babu zetu. 


Kanuni ya Tano


Uwezo wa kuchambua, kulinda na kujielimisha unahamasishwa, kuelendelezwa, kuhifadhiwa, kutunzwa na kutangazwa kama nyenzo kuelekea kupatikana kwa amani na maendeleo. Na pia kuelekea ulinzi na maendeleo ya thamani yetu. Kupitia elimu na maendeleo ya asili yetu na stadi za maisha tulizojifunza, wana Hip Hop wana hamasishwa kila mara kufanya kazi kuwasilisha vyema mawazo yao na kufanya kazi kwa bidii.

Kanuni ya sita

Utamaduni wa Hip Hop hautambui, uhusiano, mtu, tukio, kitendo au vinginevyo, ambapo utunzwaji na maendeleo mengine ya utamaduni na vipengele vyake havizingatiwi wala kuheshimiwa. Hip Hop katu haishiriki katika matukio ambayo wazi kabisa yanavuruga au kuhatarisha uwezo wake wa kuchochea amani.Wana Hip Hop wanashauriwa kufanya biashara halali na yenye uadilifu katika makubaliano yao na kufanya malipo. 


Kanuni ya saba

Asili na lengo la Hip Hop ni zaidi ya burudani, utamaduni wa Hip Hop unaweza kuchangia upatikanaji wa pesa, heshima, mamlaka, chakula, makazi, taarifa na rasilimali nyingine.Utamaduni wa Hip Hop hauwezi kukunuliwa au kuuzwa, na pia hauwezi kuhamishwa au kubadilishana kwa kitu chochote au mtu yoyote kwa fidia au bidhaa yoyote mahala popote. Hip Hop ni utamaduni usio na bei na haununuliki, upo kwa ajili ya sisi kujikwamua kimaisha hivyo Hip Hop sio bidhaa. 

Inaendelea……… ...…… ..

Leave your comment