NEW MUSIC: Kazi Yangu Mpya na Diamond Itawatoa Kijasho Mashabiki – Saida Karoli

Msanii wa muziki wa asili, Saida Karoli amedai baada ya kupokelewa vizuri kwa wimbo wake ‘Urugamba’ anajipanga kuachia wimbo wake mpya akiwa na Diamond pamoja na Belle 9.

Muimbaji huyo amedai kibao cha ‘Urugambo’ amekitoa kama kifungua kinywa, badala yake watanzania watarajie kupata nyimbo kali mfululizo.

Saida anasema nyimbo zinazofuata ni zile alizoimba akiwashirikisha Belle 9 na Diamond Platinumz.

“Urugambo nimetoa kama zawadi kwa Watanzania, niliona nijitambulishe kama chai ya asubuhi, lakini watarajie mambo makubwa kwani hivi karibuni mimi na Belle 9 tutatoa kazi ambayo itawatoa jasho mashabiki wa muziki,” alisema Saida.

Pia muimbaji huyo amedai kwa sasa atahakikisha anaachia nyimbo nyingi kali ambazo zitamuweka vizuri katika tasnia ya muziki.

Source:bongo5.com

Leave your comment