ALBUM YA "IBADA" MBIONI KUKAMILIKA

Msanii wa nyimbo za injili Nancy Mwakahesya amesema ya kwamba album yake aliyoipa jina la IBADA,ipo mbioni kukamilika ambapo mpaka sasa tayari amesharekodi nyimbo nne katika studios za FLEXIBLE ENTERTAINMENT zilizopo sinza,legho jijini Dar es salaam.Album hiyo ambayo itabeba nyimbo nane,yote amesema ataitengeneza katika studio hizo za Flexible Entertainment.
Nancy amesema mpaka sasa ameshashaziachia nyimbo zake nne,ambazo unaweza kuzisikiliza kupitia account yake ya mdundo,unachotakiwa kufanya ni kuingia katika website ya mdundo na kuandika jina NANCY MWAKAHESYA,hapo utaziona nyimbo zake zote na kusikiliza na kuweza ku download.

Leave your comment