Nimekuja kuwachana, Ayasema Rosa Ree from the Industry

Baada ya muda mrefu wa ukimya na maandalizi hatimaye Lebo ya The Industry iliyo chini ya umiliki wa kundi la Navykenzo, yaachia ngoma ya msanii wao,Rosa Ree iitwayo "one time(mother***)"
Msanii huyo wa kike afanyaye mziki wa hip hop asema kuwa amekuja kuwachana marapa wenzake na kuwahimiza kupiga hatua nyingine kwenye mziki wa rap ili kuweza kuufikisha mziki huo kwenye matawi ya juu nchini na hata duniani. Asisitiza kwamba wasanii wa hip hop wametulia sana na wanatakiwa kuongeza juhudi ili waweze kutambuliwa zaidi na mziki huo kusambaa na kueleweka nyumbani na hata nchini zingine.
Rosa Ree aendelea na kusema kuwa watu hawatakiwi kudharau jinsia ya kike kwenye mziki wa rap na kwamba wanawake pia wanaweza kuwa marapa bora kwa hiyo waendelee kukaza.

Leave your comment