TANZANIA: Mwanzo nilikuwa nasaidiwa na wazazi wangu - Jux

 

Msanii wa bongo fleva Juma Jux anayetamba kwa sasa na ngoma yake ya 'Wivu' amesema kabla hajafanikiwa kimuziki alikuwa akitumia vitu vya nyumbani kwao kusumbua na kuuzia sura mjini.

Jux ameweka wazi kuwa hapo mwanzo alikuwa akitamba mjini kwa mali za wazazi wake ila kwa sasa hawezi kufanya tena hivyo bali anapambana kiume kwa kulipa kodi na kujiwekeza kimaisha.

Akiongea na eNewz, Jux amesema “Kwa sasa nina duka nalipa kodi ya nyumba nina gari naliangalia na pia nimepanga nyumba nalipa kodi, mwanzo nilikuwa nasaidiwa na wazazi wangu hapo nyuma na kila mtu anapenda kusaidiwa"

Hata hivyo mbali na kupitia maisha ya kutegemea vya 'bwerere' toka kwa wazazi, Jux hajaona kama ilikuwa tatizo bali ameshauri wazazi wengine waweze kuwasaidia watoto wao ili waweze kufikia malengo yao kwa kila namna.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news