TANZANIA: Ben Pol, amezungumzia juu ya kuvuja kwa wimbo wake aliomshirikisha Nameless

 

 

Msanii wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Ben Pol, amezungumzia juu ya kuvuja kwa wimbo wake aliomshirikisha Nameless kutoka nchini Kenya.

Akizungumza ndani ya eNewz, Ben Pol alifunguka kuhusu kushangaa kuiona ngoma hiyo kwenye blogs mbalimbali wakati hajaiachilia yeye wala Nameless.

 

 

“Mimi mwenyewe nimeshangaa kuuona wimbo kwenye mitandao na blog mbalimbali lakini hata nilipomuuliza Nameless alisema hafahamu chochote hata 'producer' wa ngoma hiyo Sappy alisema hahusiki kuhusu kuiachia hiyo ngoma”

 

Hata hivyo Ben Pol amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye group lao la whatsapp bado wanajadili ni kitu gani wafanye ili kuweza kuendeleza hiyo ngoma huku akisema hadhani kabisa kuwa Nameless anahusika kwa kuvuja kwa ngoma hiyo kwakuwa hatafuti kick “Nameless ni mtu mzima ambaye ana familia na anajiheshimu hawezi kufanya hivyo kwakuwa hatafuti kick” Alisema Ben Pol.

 

Alimalizia kwa kusema kwamba wimbo wa 'Yamenikuta' ni ngoma ambayo imeachiwa mitandaoni wakati akiwa 'busy' sana na project ya wimbo wa Moyo Mashine hivyo hakuweza kufatilia kwa karibu ni nini cha kufanya.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news