TANZANIA: Umefikia wakati wa kila kijana kupambana – Rama Dee

 

 

 

Msanii wa muziki wa R&B nchini Rama Dee amewataka vijana kuacha kufuata ndoto za watu wengine bali wanatakiwa kuangalia ni vitu gani wanavipenda na kuvifanyia kazi kama njia moja wapo ya kupambana na maisha na kufikia ndoto zao katika maisha.

Rama Dee ametumia mitandao yake ya kijamii kufikisha ujumbe huu kwa vijana mbalimbali ambao wanahitaji kujikomboa katika maisha ya kila siku, hivyo amewataka kuacha kukaa vijiweni na kuanza kuwachambua viongozi mbalimbali kwani kufanya hivyo bila kufanya kazi ni kujirudisha nyuma, ukizingatia hao viongozi wanaowajadili wapo kazini na wanaendelea na kazi zao.

"Umefikia wakati wa kila kijana kupambana ili kushinda mapambano ya kuifikia ndoto yako na malengo, nashukuru nimepata marafiki wazuri sana, wenye kujituma na kujielewa. Kitu rahisi katika maisha angalia kitu ukipendacho na ukiwezacho kukifanya, usifuate ndoto za watu utaishia njiani lazima, aidha utaumia" aliandika Rama Dee

Mbali na hilo Rama Dee alisema kukaa kijiweni na kuwachambua watu pasipo kufanyakazi ni tatizo ila harakati nzuri ni zile za kupigana na maisha yako ili uweze kutoboa katika maisha ya kila siku.

"Unamchambua Kikwete kwa miaka yote 10 ukiwa kijiweni, leo umeanza na Magufuli tena. Ila kumbuka wao wapo kazini pale, na wanalipwa mshahara, kijana mwenzangu 'please' fanya mambo yako, harakati nzuri ni kupambana kutimiza ndoto yako, mwana harakati mwenye kusema anafanya harakati huku akipokea mshahara serikalini na kulinda familia yake huyo sio mwanaharakati, nafikiri ni mfanyakazi kama wafanya azi wengine tu". Alimaliza Rama Dee

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment