TANZANIA: Vanessa Mdee atajwa kuwania tuzo za Nigeria Entertainment Awards

 

 

Msanii wa Bongofleva Vanessa Mdee jina lake limeingia kwenye headlines baada ya kutajwa katika moja kati ya tuzo kubwa Nigeria Entertainment, Vanessa ametajwa kuwania tuzo zinazoitwa Nigeria Entertainment Awards.

Jina la muimbaji Vanessa Mdee limetajwa katika kipengele cha kuwania tuzo ya muimbaji bora wa kike, katika kipengele hicho Vanessa anawania tuzo hiyo na wasanii wengine saba kutoka nchi mbalimbali, Nigeria Entertainment Awards zitafanyika New York Marekani, September 4 2016.

 

 

 

Waliotajwa kuwania tuzo hiz katika kipengele cha msanii bora wa kike ni Efya wa Ghana, Lira wa South Africa, MZ Vee wa Ghana, Sheebah wa Uganda, Knowless wa Rwanda, Victoria Kimani wa Kenya, Adiouza na Vanessa Mdee wa Tanzania

 

Chanzo: Millard Ayo

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment