TANZANIA: Hatuwezi kushuti video the same same video kila siku - Gnako

 

Msanii wa Bongo fleva G Nako amefunguka dhidi ya wanaodai kuwa hafananii na video aliyoenda kuishuti kwa Hascana baada ya kuikataa iliyokuwa imefanywa na Nisha.

Akizungumza na Enewz G Nako amesema kuwa kuna kitu ambacho watu wamekizoea ambacho si lazima kiwepo kwenye tasnia, hivyo watu wanatakiwa wawe tayari kupokea mapokeo ya vitu tofauti tofauti kwakuwa sanaa inakuwa kubwa hivyo inabidi kuendana na ukubwa huo.

“Hatuwezi kushuti video the same same video kila siku haziwezi kuwa video zinazofanana hii video ukiiona ni moja kati ya video ambazo ziko tofauti na ambazo uliwahi kuziona kwenye industry na ndo tofauti ambazo tunatafuta siku zote"

Nako ameendelea kusema "Kila mtu anakuwa na mapokeo yake lakini mwisho wa siku ni sanaa na sanaa inaweza ikachukua hata miaka sita kuja kuelewa kitu ambacho mtu amefanya leo mimi vision yangu ambayo nilikuwa nayo ndiyo hiyo ambayo nilikuwa nataka kuiwasilisha”, alisema G Nako.

 

Unaweza kutazama video zote mbili hapa:

 

"Arosto" - Iliyotengenezwa na Nisher

 

"Arosto" - Iliyotengenezwa na Hascana

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

Leave your comment