TANZANIA: Diamond aitambulisha rasmi label ya WCB

 

Leo June 2, 2016 label ya Wasafi inayomilikiwa na staa Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz inaingia kwenye headlines za Bongo Fleva baada ya kumtambulisha rasmi  msanii  wao mpya  Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne atakayesimamiwa kazi zake katika label hiyo.

Kwa mujibu wa Diamond Platnumz amesema… “Kwasasa Label yangu inakuwa na jumla ya wasanii wanne ukiachana na Rich Mavoko kuna Dada yangu Queen Darling ambaye sijawahi kumtambulisha lakini anakuwa ni msichana wa kwanza katika label yangu kwahiyo tutakuwa na Raymond, Harmonize, Rich Mavoko na Queen Darling” Diamond Platnumz

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa, Godfrey Mngereza ambaye alizungumza na kumpongeza Diamond huku akiwataka wasanii wengine kushirikiana kwa namna hiyo.

 

 

 

 

 

Unaweza  kutazama hapa tukio hilo la kutambulishwa rasmi lebo ya WCB na kusainishwa kwa Rich Mavoko

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment