TANZANIA: Kuimba live ni gharama sana – Grace Matata

 

Msanii Grace Matata ambaye anafanya poa kwenye muziki wa live na band jukwaani, amefunguka sababu ambayo wasanii wengi wanashindwa kufanya muziki wa aina hiyo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Grace Matata amesema wengi wanashindwa kufanya muziki wa live jukwaani, kutokana na kushindwa kumudu gharama zake.

“It's a very expensive thing to run (Ni kitu ngumu sana kuendesha) uwe na band ambayo utaweza kuimantain, ukaweza kuwalipa watu, kuna vitu vingi sana vinainvolve kwenye kufanya perfomance za live, kuliko kufika na Cd yako with ur high heels ukaimba on top ukaondoka, kwa watu wengi inakuwa ngumu” alisema Grace Matata.

Grace Matata amendeelea kwa kusema kuwa hata yeye alipoanza ilikuwa ngumu kwake, lakini uongozi aliokuwa ano ndio umefanikisha kumfikisha hapo, na amekubali kuwekeza kwenye band.

“Nashukuru Mungu nimepata suport sana kama kuna watu ninaofanya nao kazi ambao wanajua, mimi nilivyoanza kabisa I remember the first time kupanda stejini nilikuwa naogopa kupita maelezo, lakini nina suport system nzuri sana na nimekubali kujiinvest”, alisema Grace Matata.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment