TANZANIA: Mke wangu alinipa tatizo la kisaikolojia – Akili The Brain

 

Msanii na producer Akili the Brain amesema kuwa kitendo cha kuachana na mke wake wa pili kilimuharibu kisaikolojia, na ndio kilichosababisha apotee kwenye game kwa muda

Akili ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa alimpenda sana mke wake huyo ambaye kwa sasa wamechana, lakini alikuwa na tatizo kubwa la kisaikolojia baada ya kuachana naye.

“Nilikuwa na mke wa pili, sasa ilikuwa chembe chembe zimebaki za mapenzi, nilikuwa naumia zaidi, yani aliniharibu kidogo kisaikolojia kwa upande wangu, nilikuwa sikumbuki watu vizuri hata naweza nikakuona wewe mpaka ukajitambulisha we nani, sa hivi tushaachana karibu miaka 6 sasa inaenda, lakini baada ya kuacha nilipata stress sana kwa sababu ya mapenzi yale, nilikuwa nampenda sana”, alisema Akili the Brain.

Akili amesema kitendo hicho kilifanya afikie hatua ya kushindwa kufanya kazi, hata show alishindwa kuzifanya pia, lakini anamshukuru Mungu kwani kwa sasa yupo sawa.

“Ilini-affect sana akili yangu, nilikuwa sifanyi kazi vizuri, hata nikienda kwenye perfomance zangu sifanyi kazi vizuri nakuwa mnyonge mnyonge lakini Mungu kanisaidia imeenda ime-heal”, alisema Akili the Brain.

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment