TANZANIA: “Juma Nature anianche nifanye kazi” – KR Mullah

 

 

Akiongea na East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo, KR Mullah amemtaka Juma Nature amuache kwa sasa afanye kazi, kwani kwa sasa anataka kubadilisha ladha ya muziki wake na huenda hajapendezwa na yeye kuingia Radar Entertainment na kuachana na Wanaume Halisi.

“Nilikuwepo ndani ya kundi la wanaume halisi, sasa labda anavyoona mi nipo huku inamaana ye anaona kazi zake tena zitakuwa zinalega lega, pengine labda hakupendezewa mimi kwenda kufanya kazi na yule mtu na kwamba yeye alitegemea mi nifanye kazi naye, siku zote wanasemaga watu ni kubadilisha mazingira, kubadilisha sanaa, kikubwa aniache nitingishe tu aniache', alisema KR Mullah.

 

KR Mullah akiwa na TID

 

Pia KR amemuongelea TID ambaye Juma Nature alimtahadharisha kuwa makini nao wasije wakamuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, kwani msanii huyo alishawahi kuwa na kashfa ya matumizi ya madawa ya kulevya na kusema kwa sasa hajamuona kutumia vitu hivyo. “Kusema kweli zamani muda uliopita nilikuwa nasikia sikia hizi taarifa, lakini yeye mwenyewe alitangaza kuacha muda mrefu, lakini kwa sasa tangu nimeanza kukaa naye sijawahi kumuona akiitumia au akifanya hayo mambo, muda mwingi tunapiga stori za kikazi zaidi” alisema KR Mullah.

 

 

Chanzo: Enewz

 

 

 

Leave your comment

Other news