TANZANIA: Juma Nature ampa onyo KR Mullah

 

Mkongwe wa muziki Tanzania Juma Nature amempa onyo kali rapper KR Mulla baada ya kugundua kuwa ameanza kuroll na TID.Kwenye mahojiano ya mwisho kati ya KR Mulla na eNewz, KR alijitambulisha kama Raisi wa Radar Entertainment, ambayo inamilikiwa na TID, na siku za karibuni TID na KR wameonekana kuwa marafiki ukiachilia mbali kufanya kazi pamoja ndani ya Radar Entertainment.

Juma Nature ambaye aliwahi kufanya muziki ndani ya kundi la Wanaume Family pamoja na KR Muller ameamua kumpa onyo KR asije akashawishiwa na swahiba wake TID kuanza kutumia madawa ya kulevya yaani "Unga". kutokana na stori zilizozagaa mjini kumjumuisha TID kwenye orodha ya wasanii wanaotumia madawa ya kulevya. Zaidi Juma Nature alikataa kukubali kuwa KR ni Raisi wa Radar Entertainment kwa kuiambia eNewz kuwa "Hata huyo TID mwenyewe sio Rais, sasa KR ni Rais wa wapi? Rais ni Magufuli tu". Alisema Msitu wa Vina Juma Nature

 

 

Chanzo: Enewz

 

 

 

Leave your comment

Other news