TANZANIA: “Style yangu ni kimyakimya, sitaki Kiki” - Chege

 

Siku hizi kwenye maisha ya mastaa wengi wa dunia, huwa kuna zile stori wanazitengeneza wenyewe kwa sababu maalum ili kufanya majina yao yaendelee kutajwa kwenye media kila wakati au wakati mwingine wakiwa wanajiandaa kuachia nyimbo au movie mpya ambapo hata Tanzania wapo baadhi wanaoaminika kufanya hivyo yaani ‘kutengeneza kiki’

 Kuhusu hii ya kutengeza ‘kiki‘ Chege ambaye alikaa kwenye OnAIR with Millard Ayo amesema , “Ni mipango unajua kila mtu ana staili yake ya kutoka, kuna mwingine anatoka kwa ukimya hataki stori nyingi… wewe utasikiliza tu kazi yake, ni staili tu na sio kitu kibaya kama inaongeza kitu kwenye game yake, kama inapunguza inabidi kuangalia njia nyingine”

Itakuja siku moja Chege atengeneze kiki? Akasema, “staili yangu itabakia hiihii ya kufanya kimyakimya bila kelele nyingi, siwezi kubadilika nikawa mtu wa kutengeneza kiki… sio mimi tu ila TMK hatuna hizo ingawa sio kitu kibaya, inategemea tu na wewe umejitengeneza kwenye mtoko wako”

 

Chanzo: Millard Ayo

Leave your comment