TANZANIA: ‘Zigo Remix’ ya AY na Diamond kuruhusiwa kuonyweshwa usiku na TCRA

 

Video ya ‘Zigo Remix’ ya msanii AY akiwa na Diamond baada ya kukatazwa kuonyweshwa sasa ni ruksa kuchezwa usiku kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

TCRA imetoa taarifa hiyo kwenye mtandao wa Twitter wakati ikijaribu kumwelewesha AY pamoja na mashabiki wenye duku duku kuhusiana na uamuzi huo. Awali uamuzi wa TCRA ulitafsiriwa na kuwa video hiyo yenye views zaidi ya milioni 2.7 You Tube imepigwa marufuku kabisa kuoneshwa kwenye TV za Tanzania.

Leave your comment