Mafanikio makubwa kwa Mdundo! Downloads Millioni 8 Watumiaji zaidi ya Milioni 2.3 kwa Mwaka 2015..

Kama mdundo tunaamini katika tamaduni ya uwazi na ukweli, hivyo basi tunakushirikisha wewe kama mdau na msanii kujua taarifa muhimu za wasanii wetu na watumiaji mbalimbali wa mdundo.com/

Kuongezeka kwa namba ya watuamiaji

Kwa miaka 3 mdundo imekuwa ikiendeshwa ndani ya nchi (Kenya) na kuwekeza kiasi cha milioni 65, huku namba ikiwa inazidi kukua.

Jumla ya wasanii 15,000 wamejiunga na Mdundo kutoka nchi 36 tofauti. Kwa sasa wanaupload nyimbo zao karibu kila siku.

Kwa kila siku kwa mwaka 2015 si chini ya nyimbo 50 zimekuwa zikiwekwa Mdundo.

Watumaiaji wa Mdundo pia wameongezeka, kwa mwaka 2015 namba imeongezeka hadi milioni 2. Na hii inaendelea kukua siku hadi siku kadri ya tunavyoongeza taarifa muhimu juu ya utumiaji wa App ya Mdundo.

Tumekuwa na jumla ya watumaiji milioni 8 na wasanii 9,000 waliojiunga nasi.

Jinsi gani wasanii wanafaidika na Mdundo

‘Download zinapokuwa nyingi pia na kiasi cha hela kinaongezeka’

Kupitia matangazo Mdundo inakusanya mapato, na kisha pesa hiyo kugawanywa 50/50 na wasanii wetu.

Kwa ujumla kama Mdundo ikipata mapato mengi zaidi mwaka huu ni wazi pia na wasanii watapata kipato kingi zaidi kuliko mwaka uliopita.

Mdundo inafanya kazi na makampuni mbalimbali na kuweka matangazo yao na kwenye myimbo za wasanii. Hivyo wasanii kupitia downloads wanapata kipato.

Pia tunawapa tuzo wasanii wetu kutokana na namba ya downloads walizopata. Na zimegawanyika katika vipengele 3;

01-Mdundo Platnum – 1 million downloads

02- Mdundo Gold – 500,000 downloads

03- Mdundo Silver – 100,000 downloads

04- Mdundo Bronze (shaba) – 50,000 downloads

Hata hivyo hakuna msanii yeyote aliyeweza kupata tuzo ya Platnum au Gold, kati ya wasanii waliopata tuzo ya Mdundo Silver ni Avril, Bahati, Willy Paul, H_Art Band, Sauti Sol, Rhymaholic MVi na wengineo.

Msanii anawezaje kukua kupitia Mdundo

“Mdundo ni sehemu nzuri kwa msanii anaechipukia na mwenye nafasi ndogo ya kufikia mashabiki wake. Ni mahali rahisi kuweza kudownload nyimbo na kufikia mashabiki pia…”

 

Huu ni ushuhuda toka kwa msanii Rhymaholic MVI, jina ambalo si maarufu katika vyombo vya habari lakini bado kama msanii mchanga ameweza kuwa kati ya wasanii wenye download nyingi zaidi Mdundo.

Akiwa kati ya waliopata tuzo ya Mdundo Silver, inamaanisha kuwa Rhymaholic MVI alipata 100,000 downloads, ambapo pia msanii yeyote chipukizi anaweza kupata kama yeye.

Lakini ana siri ambayo imemuwezesha kupata mafanikio hayo ambayo ni mitandao ya kijamii.

“Nina timu ambayo inanisaidia kutangaza muziki wangu kwenye mitandao ya kijamii. Nina group la Facebook linaitwa Rhymaholic MVI (lenye zaidi ya followers 7,000) na nimemsign Lil Felly, tunafanya kazi pamoja na kusaidiana kupromote nyimbo zetu”.

“Media za kawaida si njia pekee ya kujitengenezea jina. Ni vigumu kwa Dj kupiga nyimbo za msanii mchanga kwenye TV au Redio, lakini Wakenya wengi wapo kwenye mitandao ya kijamii na ukipata mashabiki wengi huko ni rahisi pia kupata exposure kwenye radio na TV”

Hivyo ni rahisi kutengeneza career kwenye muziki, kula, kunywa, ishi na unaweza kuendesha gari ukiwa ndani ya Mdundo.

Kwa vyovyote vile haijalishi mahali ulipo ndoto zako ni halali ‘No matter where you are from, your dreams are valid –Lupita Nyong’o”.

Leave your comment