05- EXCLUSIVE (TANZANIA) – Hii ndo sababu ya wasanii kujiingiza kwenye kuuza na kutumia unga – Wakazi

 

Msanii wa hiphop nchini ameeleza sababu za wasanii kujiingiza katika suala zima la kuuza na kutumia madawa ya kulevya (unga). Ambapo amesema wasanii wa Tanzania huingia katika mkumbo huo kutokana na kuiga aina fulani ya maisha.

Akizungumza katika kipindi cha mkasi TV kinachorushwa na EATV, wakazi amedai licha ya tabia hiyo ya kugeza bado anafanya utafiti ili kujua zaidi.

“Bado ilo suala nalifanyia utafiti sio tu muziki bali entertainment na drugs”, alisema. “Kwasababu Watanzania wana tabia moja ya kugeza, mtanzania akisikia kitu fulani kimekiki nje kila mtu anakigeza. Sasa sisi Watanzania tuna tabia ya kushobokea vitu labda hii ndio kitu kinasababisha issue za drugs zikaja”, aliongeza.

“Halafu sio tu upande wa matumizi kuna hili suala nasikia watu wanajihusisha kabisa kwenye biashara yenyewe, sawa mtaani hali ni ngumu kwahiyo mtu kuingia huko siwezi kumshangaa sana. Kwahiyo hicho kitu nimejaribu kufanyia uchunguzi sipati jibu kwasababu wengine wanasema wasanii wanakuwa na stress wanaamua kutumia madawa lakini kuna wengine hawajawahi kupata stress na wanaamua kutumia madawa halafu ndio anasema ngoja nikaimbe”.

Leave your comment